Tuesday 4 October 2016

NIDA WAANZA KUSAJILI NA KUHAKIKI WATUMISHI WA UMMA WILAYANI SERENGETI

Habari kutoka Kitengo cha Habari na Mawasiliano - HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI.


Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA, imeanza kusajili watumishi wa taasisi za Serikali Wilayani Serengeti kwa kutumia mfumo wa kieletroniki kwa lengo la kutoa vitambulisho vya taifa. Aidha zoezi hilo linaenda sambamba na kubaini watumishi hewa pamoja na utambuzi wa vyeti halisi na vya kughushi vya elimu na taaluma.


      Ofisa wa NIDA Fred Mwasipu (kushoto) akiwa anakagua vyeti vya mtumishi mapema jana katika zoezi la uhakiki.

Zoezi hilo litakalofanyika kwa watumishi wa umma wote ndani ya Wilaya ya Serengeti, limefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu nje ya ofisi yake ambapo watumishi wa umma kutoka taasisi mbali mbali za serikali walihudhuria. "Nashukuru mmefika kufanya kazi hii kubwa hasa katika kipindi hiki ambacho serikali inapambana na watumishi hewa na wenye vyeti feki" alisema Babu, aidha ameiomba NIDA kufanya kazi hiyo kwa weledi na kuhakikisha suala la watumishi hewa linaisha serikalini.

Mheshimiwa Babu amewaagiza watumishi wote wa taasisi za serikali kuhakikisha wanawasilisha nyaraka zote muhimu zinazohitajika kwa zoezi hilo na kufanyiwa usajili na maofisa wa NIDA ndani ya muda wa siku 14 zilizotengwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Juma Hamsini ambaye naye pia alihudhuria ufunguzi wa zoezi hilo, ameishukuru Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kwa kufika Serengeti na kufanya zoezi hilo na kuwataka watumishi kutoa ushirikiano na kuondoa hofu iliyokuwepo awali kuhusu shughuli hiyo.

Aidha Msajili Mkuu wa NIDA Wilaya ya Serengeti, Bw. Fred Mwasipu alizitaja changamoto alizozibaini katika hatua ya awali ya ujazaji wa taarifamuhimu katika fomu, ambazo ni; Uwepo watumishi ambao wana vyeti vinavyoonyesha kuwa wamezaliwa Wilaya ya Serengeti ilihali si kweli,Watumishi kubadili majina, kutokuwa na vyeti halisi huku watumishi wengine wakiwa hawana nyaraka muhimu zinazohitajika. Aidha Mwasipu amewaomba watumishi wote kuhakikisha kuwa wanahakikiwa vyeti vyao vyaelimu na taaluma. “Zoezi hili linaenda sambamba na uchukuaji wa taarifa muhimu zitakazotumika katika utengenezaji wa vitambulisho wa taifa”alisema Mwasipu.

Katibu Tawala Wilaya ya Serengeti, Cosmas Qamara alitoa maelezo kuhusu utolewaji na upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa ambapo alisema “Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Serengeti haitoi vyeti vya kuzaliwa kwa mtu yeyote aliyezaliwa nje ya Wilaya ya Serengeti” Qamara amewataka watumishi kuacha kufanya udanganyifu wa mahali pa kuzaliwa na vyema wafike katika ofisi za Wilaya walizozaliwa ili kupata vyeti halisi au kufuata taratibu zilizowekwa na kuwaomba wenye mahitaji kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kufanya maombi ya kupata vyeti hivyo kulingana na Wilaya walizozaliwa.

Zoezi la usajili wa watumishi wa umma na uhakiki wa nyaraka kwa kutumia mfumo wa kieletroniki, linatarajiwa kuchukua muda wa wiki mbili ambapo maofisa wa NIDA wataweka kambi katika Tarafa 4 ili kuleta ufanisi wa kazi na kuwafikia watumishi wa umma walio mbali na makao makuu ya Wilaya yaliyopo katika Mji wa Mugumu.

                    MATUKIO YALIYOJIRI KATIKA PICHA

  


    Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Nurdin Babu (kushoto) akihakikiwa na Ofisa wa NIDA.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Juma Hamsini (kushoto) akihakikiwa na Ofisa wa NIDA.

   Katibu Tawala Wilaya ya Serengeti  Cosmas Qamar(kushoto) akihakikiwa na Ofisa wa NIDA.

   Watumishi wa Umma wakiwa tayari kwa ajili ya uhakiki.

 
   
   



1 comment:

  1. How to use the $100 welcome bonus at the Hard Rock Hotel
    The 경산 출장마사지 Hard Rock Hotel & 화성 출장샵 Casino in Highland, California offers a huge welcome bonus 경기도 출장안마 for new players 천안 출장샵 who register an account at any Hard Rock 포항 출장샵 casino.

    ReplyDelete