Thursday 23 March 2017

Tovuti rasmi ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kupitia Kitengo cha TEHAMA & UHUSIANO inapenda kuutarifu umma kuwa kwa sasa habari zote na matukio ya picha na video zitapatikana kupitia tovuti rasmi ya taasisi (www.serengetidc.go.tz)

Katika tovuti hii, umma unaweza pia kupakua nyaraka mbali mbali  ili kurahisisha utendaji wa kazi kwa muda mfupi zaidi.


Imetolewa na

Englibert Kayombo
Afisa Habari & Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
23 Machi 2017


Tuesday 31 January 2017

KITUO CHA AFYA NATTA CHAPATA GARI MAALUM LA WAGONJWA (AMBULANCE)

Habari kutoka Kitengo cha TEHAM & UHUSIANO
HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENEGTI

Serikali Wilayani Serengeti Mkoa wa Mara yaikabidhi Kituo cha Afya Natta Gari maalumu ya kuwahisha wagonjwa (ambulance). Makabidhiano ya gari hilo yamefanyika siku ya jana tarehe 31 Januari 2017 nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti. Akikabidhi gari hilo Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Nurdin Babu ameitaka Idara ya afya Wilayani kuboresha upatikanaji wa huduma ya haraka ili kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na ukosefu wa huduma ya haraka.
Gari maalumu Kwa ajili ya kubeba wagonjwa (Ambulance) lilitoloewa na Wizara ya Afya Kwa ajili ya kuboresha huduma za matibabu katika Kituo cha afya cha Natta Wilayni Serengeti.




Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Mhe. Nurdin Babu (katikati) akikabidhi kati ya gari kwa Diwani wa Kata ya Natta Mhe. Juma Porini Keya (kushoto) 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambae pia ni Diwani wa Kata ya Natta, Mhe Juma Porini Keya akishukuru Wizara ya afya kwa kufanikisha upatikanaji wa Gari hilo

DC Nurdin Babu akijaribu kuwasha gari hilo.

Wednesday 30 November 2016

KIJIJI CHA NYAMISINGISI WILAYANI SERENGETI KUANDAA NA MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI.

Habari toka Kitengo cha TEHAMA & UHUSIANO
HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI.

Kijiji cha Nyamisingisi kilichopo Kata ya Issenye Wilayani Serengeti katika Mkoa wa Mara kunufaika na mpango wa matumizi bora ya ardhi.


 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ikishirikiana na wadau wake wa maendeleo; Shirika la Hifadhi ya Serengeti (SENAPA) pamoja na Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS) kupitia ufadhili wa Benki ya Wananchi wa Ujerumani(KfW) wamejikita katika kuhakikisha vijiji vilivyo karibu na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti pamoja na pori la akiba la Grumeti na Ikorongo kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi.  “Tunashukuru kwa kupata fursa hii, mpango huu ni mojawapo ya kipaumbele kikuu katika kijiji hiki” alisema Diwani wa Kata ya Issenye Mhe. Mosi Nyarobi alipokuwa akiwakaribisha wajumbe wa timu ya matumizi bora ya ardhi ya Wilaya ya Serengeti katika kikao kilichofanyika na Serikali ya kijiji hicho leo tarehe 30 Novemba 2016.

Aidha wanakijiji kwa kauli moja kupitia mkutano maalum wa Kijiji uliofanyika siku hiyo hiyo wameridhia kuundwa kwa kamati ya mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji yenye wajumbe nane. Kamati hiyo kwa kushirikiana na Serikali ya Kijiji kwa pamoja itaandaa rasimu ya mpango wa matumizi bora ya ardhi ya Kijiji cha Nyamisingisi.









Wednesday 23 November 2016

MATUKIO KATIKA PICHA: H/W SERENGETI WAANDAA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO.

Waheshimiwa Madiwani, Wadau wa Maendeleo pamoja na Wataalamu kutoka taasisi za Serikali Wilayani Serengeti waupitia mpango mkakati wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti utakaomudu kwa miaka mitano kuanzia mwaka wa bajeti 2016/17 mpaka 2020/21. “Bila mpango mkakati huu hakuna maendeleo” amesema Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mheshimiwa Nurdin Babu alipokuwa akifungua kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 22 Novemba 2016.














Monday 31 October 2016

SERENGETI NA BUNDA ZANUFAIKA NA UWEKEZAJI WA SINGITA GRUMETI.

Habari toka Kitengo cha TEHAMA & MAHUSIANO
HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI.

Mfuko wa Singita Grumeti umeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuboresha hali ya elimu katika Wilaya za Serengeti na Bunda.
Hii imedhihirika kwenye halfa ya kukabidhi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa ili kupunguza uhaba wa madawati katika Wilaya hizo. Aidha Grumeti wamekabidhi nyumba ya kuishi mwalimu iliyojengwa katika Shule ya Msingi Makundusi.

Mkuu wa Huduma za Jamii Singta grumeti Richard Ndaskoi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda katika hafla  iliyofanyika  Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti.
“Tuko hapa kukabidhi madawati haya 500 yenye thamani ya Tshs. Milioni 112 kwa Wilaya za Serengeti na Bunda pamoja na nyumba hii yenye thamani ya Tshs. Milioni 86” alisema Richard Ndaskoi ambae ni Mkuu wa Huduma za Jamii toka Mfuko wa Singinta Grumeti.
Akipokea misaada hiyo, Dk. Mlingwa alisema “Nawashukuru Singita Grumeti kwa Msaada huu wa madawati pamoja na nyumba hakika mchango wenu katika Mkoa wa Mara unaoneka” Dk Mlingwa amewataka wawekezaji wengine katika Mkoa wa Mara kuchangia madawati katika Wilaya za Serengeti na Bunda kwani bado zina uhaba wa madawati. 
Aidha Dk. Mlingwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa kuwa na mahusiano mazuri na wawekezaji waliopo katika Wilaya hiyo “Tukiwawekea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao hata wananchi pia watanufaika na uwepo wa wawekezaji hawa” alisema Dk. Mlingwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili wote kwa nyakati tofauti wameushukuru Mfuko wa Singita Grumeti kwa msaada huo wa madawati na kuuomba mfuko huo kuendelea kuchangia katika shughuli za maendeleo katika Wilaya za Serengeti na Bunda. “Wilaya hii ina wawekezaji wengi lakini wamekuwa nyuma katika kuchangia shughuli za maendeleo, nawapongeza kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii inayowazunguka pamoja na kuchangia katika maendeleo ya Wilaya ya Serengeti” alisema Nurdin Babu.
Aidha Bi. Bupilipili ameuomba Mfuko huo kuanzisha kampeni maalumu ya kuongeza kiwango cha ufaulu kwa watoto wa kike kwa shule za sekondari Wilayani Bunda.
Singita Grumeti wamekuwa wawekezaji wenye tija kwa wananchi wa Wilaya za Serengeti na Bunda licha ya kuwa mstari wa mbele kuchangia katika shughuli za maendeleo, kampuni hiyo pia imekuwa ikitoa ajira kwa wakazi toka wilaya hizo mbili pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi toka wilaya hizo.
Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda katika hafla  iliyofanyika  Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti.


Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa nyumba ya kuishi mwalimu yenye thamani ya Tshs Milioni 86 iliyojengwa katika Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti.


Thursday 20 October 2016

MAPATO YA MINADA WILAYANI SERENGETI YAONGEZEKA.

Habari toka Kitengo cha Habari na Mawasiliano.
HALMSHAURI YA WILAYA YA SERENGETI.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Mhe. Juma Porini Keya akitoa risiti kwa kutumia kifaa cha POS.

“Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imefanikiwa kuongeza mapato yatokanayo na minada mbali mbali inayofanyika ndani ya Wilaya”

Hayo yamesemwa na Terry Hurson ambae ni Kaimu Mtunza Fedha wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti alipokuwa anazungumza na Waheshimiwa Madiwani wanaounda Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango waliofanya ziara katika Mnada wa Kijiji cha Rung’abure kilichopo Kata ya Rung’abure.

Ziara hiyo ya ukaguzi ni mwendelezo wa taratibu zilizowekwa na Serikali kwa kuwahusisha Waheshimiwa Madiwani wanaounda Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kutembelea miradi kila baada ya miezi mitatu (Robo Mwaka wa Serikali)

Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Juma Porini Keya pamoja na Katibu wa Kamati hiyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Juma Hamsini pamoja na wajumbe wa Kamati walijionea jinsi ukusanyaji wa mapato unavyofanyika kwa kutumia vifaa vya kieletroniki (POS) vinavyotumika pia kutoa risiti za malipo. “Mapato ya Minada yameongezeka kutokana na kuzuia mianya ya ukwepaji wa kodi na matumiz ya POS” alisema Terry Hurson. Aliongeza kwa kusema "kipindi cha mzabuni mapato yatokanayo na mnada wa kijiji cha Rung'abure yalikua ni Tshs Milioni 2.4 kwa mwezi na sasa tunakusanya wastani wa Tshs Milioni 3.2"

Ukusanyaji wa mapato unafanywa na watumishi wa Serikali, hii ni baada ya Serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuzitaka Halmashauri zote nchini kukusanya mapato na kuacha kutumia wazabuni katika kukusanya mapato kwenye masoko na minada.

                                                             MATUKIO KATIKA PICHA
Kutoka Kushoto Mhe. Juma Porini Keya, katikati ni Bw. Terry Hurson (Kaimu Mtunza Fedha) kushoto ni Charles Ghati (Mkusanyaji wa Mapato) katika mnada wa Rung'abure.


Wafanyabiashara katika mnada wa kijiji cha Rung'abure wakifanya malipo.
Huduma za chakula pia hupatikana.


MAPATO YA MINADA WILAYANI SERENGETI YAONGEZEKA.

Habari toka Kitengo cha Habari na Mawasiliano.
HALMSHAURI YA WILAYA YA SERENGETI.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Mhe. Juma Porini Keya akitoa risiti kwa kutumia kifaa cha POS.

“Halmashauri ya wilaya ya Serengeti imefanikiwa kuongeza mapato yatokanayo na minada mbali mbali inayofanyika ndani ya Wilaya”

Hayo yamesemwa na Terry Hurson ambae ni Kaimu Mtunza Fedha wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti alipokuwa anazungumza na Waheshimiwa Madiwani wanaounda Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango waliofanya ziara katika Mnada wa Kijiji cha Rung’abure kilichopo Kata ya Rung’abure.

Ziara hiyo ya ukaguzi ni mwendelezo wa taratibu zilizowekwa na Serikali kwa kuwahusisha Waheshimiwa Madiwani wanaounda Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kutembelea miradi kila baada ya miezi mitatu (Robo Mwaka wa Serikali)

Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Juma Porini Keya pamoja na Katibu wa Kamati hiyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Juma Hamsini pamoja na wajumbe wa Kamati walijionea jinsi ukusanyaji wa mapato unavyofanyika kwa kutumia vifaa vya kieletroniki (POS) vinavyotumika pia kutoa risiti za malipo. “Mapato ya Minada yameongezeka kutokana na kuzuia mianya ya ukwepaji wa kodi na matumiz ya POS” alisema Terry Hurson.


Ukusanyaji wa mapato unafanywa na watumishi wa Serikali, hii ni baada ya Serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuzitaka Halmashauri zote nchini kukusanya mapato na kuacha kutumia wazabuni katika kukusanya mapato kwenye masoko na minada.

                                                   MATUKIO KATIKA PICHA
Kutoka Kushoto Mhe. Juma Porini Keya, katikati ni Bw. Terry Hurson (Kaimu Mtunza Fedha) kushoto ni Charles Ghati (Mkusanyaji wa Mapato) katika mnada wa Rung'abure.


Wafanyabiashara katika mnada wa kijiji cha Rung'abure wakifanya malipo.
Huduma za chakula pia hupatikana.