Friday 26 August 2016

WALIMU SERENGETI KUTUMIA VISHIKWAMBI (TABLET) KUTUMA TAARIFA TAMISEMI

Habari na Englibert Kayombo
 
Walimu wakuu 109 kutoka shule za msingi Wilayani Serengeti wamewezeshwa mafunzo ya utumiaji wa mfumo wa taarifa za shule (School Information System - S.I.S) kwa kutumia vishikwambi (Tablet)
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyofadhiliwa kupitia programu ya EQUIP Tanzania yalianza tarehe 25 Agosti na kukamilika 26 Agosti 2016 katika shule ya Msingi Kambarage iliyopo katika Mji wa Mugumu yamewawezesha walimu hao pia kupatiwa kishikwambi kwa kila mmoja.
Akiongea kuhusu mafunzo hayo, Mwezeshaji kitaifa wa Mfumo wa School Information System Bw. Victor Mkama alisema "Mafunzo hayo ni muhimu kwa walimu ili kuweza kutumia vishikwambi hivyo bila matatizo na kuwajengea uelewa wa umuhimu wa kutuma taarifa kwa kutumia njia ya mtandao" Mwezeshaji aliendelea kwa kusema kuwa "wametoa vishikwambi 109 kwa walimu wakuu wote wa shule za msingi wilayani serengeti vyenye thamani ya Milioni 38.1 ili kuweza kutuma taarifa muhimu zinazohusu shule waliyopo moja kwa moja TAMISEMI" Vishikwambi hivyo vitatumika katika ukusanyaji wa taarifa muhimu zikiwemo idadi ya walimu, wanafunzi, madarasa, madawati, matundu ya vyoo pamoja na nyumba za walimu na rasilimali zinazopatina katika maeneo ya shule na kutumwa moja kwa moja TAMISEMI hivyo kupunguza usumbufu wa upatikanaji wa taarifa uliokuwa ukiipata Serikali.








3 comments:

  1. ni hatua nzuri aseee...tujitahd bas hzo tablet ztuletee mabadiliko ambayo ni positv ktk upande wa elimu..hasa wilaya yetu#serengeti...ambayo imekuwa ikifanya vbaya..all da best

    ReplyDelete
  2. ni hatua nzuri aseee...tujitahd bas hzo tablet ztuletee mabadiliko ambayo ni positv ktk upande wa elimu..hasa wilaya yetu#serengeti...ambayo imekuwa ikifanya vbaya..all da best

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete