Friday 26 August 2016

VIKUNDI VYA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA HATARISHI WILAYANI SERENGETI VYANUFAIKA NA MIKOPO.

Habari na Serengeti Media Centre
(www.serengetimediacentre.blogspot.com)

Zaidi ya Tsh Milioni 308 zimekopeshwa kwa vikundi 96 vya Watoto waishio katika Mazingira Hatarishi kupitia Mradi wa Pamoja Tuwalee wilayani Serengeti Mkoa wa Mara kwa kipindi cha mwaka 2011 hadi 2016.
Mradi wa Pamoja Tuwalee ambao umefikia ukomo ulikuwa unaendeshwa na Shirika la Pact Tanzania kwa kushirikiana na asasi ya BAK-AIDS kwa ufadhili wa USAID/PEPFAR katika kata 17 kati ya 30 za wilayani hapa,na kuwezesha akina mama wengi kujihusisha na shughuli za bustani za mboga mboga ambazo zimewawezesha kuweka akiba.
Mratibu wa Mradi wa BAK-AID wilaya ya Serengeti Christopher Genya kwenye kikao cha wadau wa maendeleo wilaya wakati wa kukabidhi shughuli za mradi huo kwa  halmashauri alisema,vikundi hivyo vina akiba y ash 331,162,260,na wanaendesha biashara mbalimbali 1473 katika maeneo yao.
“Kupitia mradi huu watoto 4517 kati ya 8,046 wanalelewa na walezi walio katika vikundi,na kaya 1,839 zimenufaika na mradi huo na wameweza kuboresha makazi yao,wengine wamenunua mifugo,na waliokuwa wanakula mlo mmoja sasa wanakula milo mitatu,na mafanikio makubwa ni kwamba wanajisimamia wenyewe,”alisema.
Hata hivyo alisema katika utekelezaji wa mradi huo walikabiliana na changamoto za baadhi ya kamati za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kutokuwasaidia watoto,ikiwemo kutokushirikishwa katika vikao vya serikali za vijiji na kata.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ambaye pia ni afisa maendeleo ya jamii Sunday Wambura aliwataka wadau wa maendeleo kuhakikisha katika shughuli zao wanaweka mipango ya kuwasaidia watoto wa mazingira hatarishi,kwa kuwa hilo ni jukumu la kila mmoja.
Mapema afisa mradi huo Eza Yusuph alisema lengo kuu lilikuwa kuimarisha mifumo iliyopo ya jamii na familia zao,kuongeza rasilimali za ndani na nje katika kufikia mahitaji ya watoto na  mfumo wa ustawi wa familia baada ya kukosekana kwa msaada toka nje.


                                                         MATUKIO KATIKA PICHA

Mratibu wa mradi wa pamoja Tuwalee wilaya ya Serengeti Christopher Genya kulia akimkabidhi nyaraka za mradi huo ambao umemaliza muda wake Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya Sunday Wambura katikati ni Afisa Ustawi wa Jamii Faustine Matesi.




Wadau katika picha ya Pamoja.

2 comments:

  1. ni hatua nzuri..lakin kiuhalisia tukienda maeneo husika#kwa wahusika wenyewe...kuna vitu tunaweza vipima as a result ya hyo pesa!!??tangible results...kama zpo sawa na kama sio tujaribu kuona ni wap tunakosea..all da best kaka#sunday..nakubali utendaj wako cku zote

    ReplyDelete
  2. ni hatua nzuri..lakin kiuhalisia tukienda maeneo husika#kwa wahusika wenyewe...kuna vitu tunaweza vipima as a result ya hyo pesa!!??tangible results...kama zpo sawa na kama sio tujaribu kuona ni wap tunakosea..all da best kaka#sunday..nakubali utendaj wako cku zote

    ReplyDelete