|
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Nurdin Babu (kushoto) akisalimiana na Mgeni Rasmi wa Harambee hiyo Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Bw. William Mwakilema. |
Harambee ya
ukamilishaji wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Robanda iliyofanyika katika
majengo ya shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Robanda imefanikiwa kupata jumla ya fedha taslimu
Tsh Milioni 11,299,000 na fedha za kigeni 13 US Dollars zilipatikana papo hapo
pamoja na ahadi ya fedha kiasi cha Tshs Mil 42,499,500 fedha za kigeni 2,000 US Dollars, Mifugo Ng'ombe
watano (5), mbuzi wawili (2). Serikali ya kijiji cha Robanda imeahidi
kujenga nyumba moja (1) ya kuishi walimu huku Kampuni ya Thomson Safari ikiahidi
kujenga nyumba tatu za kuishi walimu na kuwa na jumla ya nyumba nne (4) zote zikiwa
na thamani ya Tshs Milioni 290. Mifuko ya Saruji 237 iliahidiwa kukamilisha
ujenzi wa shule hiyo kutoka kwa wadau mbali mbali wa maendeleo walioshiriki
harambe hiyo. Aidha Benki ya Posta tawi la Musoma imechangia madawati 50, huku
wadau wengine wa maendeleo kuongezea madawati manne (4) na kufanya idadi ya
madawati yaliyochangiwa kufikia 54. Akitoa shukrani za dhati Mgeni rasmi katika
harambee hiyo Mhifadhi Mkuu toka HIfadhi ya Taifa ya Mbuga ya Wanyama Serengeti
Bw William Mwakilema alisema “anashukuru wale wote walioguswa na kuchangia
ujenzi wa shule hiyo kwani kukamilika kwake kutasaidia wanafunzi waishio maeneo
jirani na robanda kuwa na shule karibu na kuondoa adha ya umbali mrefu
wanaotumia wanafunzi hao kwenda shuleni”
Harambe hiyo iliudhuliwa na Mkuu wa Wilaya ya serengeti Mhe.
Nurdin Babu, Katibu Tawala Wilaya ya Serengeti Bw. Cosmas Quamara na Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Bw. Juma Hamsini Seph pamoja na
Waheshimiwa Madiwani pia walijitokeza kuunga mkono Mhe. Diwani wa Kata ya Ikoma
Mhe. Michael Kunani huku wageni kutoka ndani na nje ya wilaya ya serengeti
walijitokeza na kufanikisha upatikanaji wa michango hiyo. Mpaka sasa shule hiyo bado haijaanza kupokea wanafunzi kutokana kutokamilika kwa baadhi ya majengo zikiwemo nyumba za walimu. kukamilika kwa majengo na uwekaji wa thamani kutaboshera hali ya elimu katika kata ya Ikoma.
MATUKIO KATIKA PICHA
|
Mhe Diwani Kata ya Ikoma Bw. Michael Kunani (kushoto) akimkaribisha Mkuu wa Wilaya Serengeti Mhe. Nurdin Babu (kati kati) kushoto ni Afisa Tarafa wa Grumet Bw, Paul Shanyangi |
|
Mhe Diwani Kata ya Ikoma (kushoto) akimkaribisha Mgeni Rasmi wa Harambee (kulia) Mhifadhi Mkuu SENAPA Bw. William Mwakilema |
|
Wadau wa maendeleo walijitokeza kwa wingi na kuchangia maendeleo kata ya Ikoma |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Bw. Juma Hamsini Seph |
|
Katibu Tawala Wilaya ya Serengeti Bw. Cosmas Quamara |
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti/ Diwani wa Kata ya Natta Mhe. Juma Porini Keya |
|
Jumla ya Tsh Mil 11,299,000 zilichangwa papo hapo. |
kazi nzur jaman...na hzo pesa zsimamiwe vzur bas ili lengo litimie...pongez kwa wadau wote wa maendeleo wilayan serengeti na wote waliofanikisha zoez hilo...
ReplyDelete