HALMSHAURI YA WILAYA YA SERENGETI.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Mhe. Juma Porini Keya akitoa risiti kwa kutumia kifaa cha POS. |
“Halmashauri ya wilaya ya Serengeti imefanikiwa kuongeza mapato yatokanayo na minada mbali mbali inayofanyika ndani ya Wilaya”
Hayo
yamesemwa na Terry Hurson ambae ni Kaimu Mtunza Fedha wa Halmashauri ya Wilaya
ya Serengeti alipokuwa anazungumza na Waheshimiwa Madiwani wanaounda Kamati ya
Fedha, Uongozi na Mipango waliofanya ziara katika Mnada wa Kijiji cha Rung’abure
kilichopo Kata ya Rung’abure.
Ziara
hiyo ya ukaguzi ni mwendelezo wa taratibu zilizowekwa na Serikali kwa kuwahusisha
Waheshimiwa Madiwani wanaounda Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kutembelea
miradi kila baada ya miezi mitatu (Robo Mwaka wa Serikali)
Kamati
ya Fedha Uongozi na Mipango inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
ya Serengeti, Juma Porini Keya pamoja na Katibu wa Kamati hiyo ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Juma Hamsini pamoja
na wajumbe wa Kamati walijionea jinsi ukusanyaji wa mapato unavyofanyika kwa
kutumia vifaa vya kieletroniki (POS) vinavyotumika pia kutoa risiti za malipo. “Mapato
ya Minada yameongezeka kutokana na kuzuia mianya ya ukwepaji wa kodi na matumiz
ya POS” alisema Terry Hurson.
Ukusanyaji
wa mapato unafanywa na watumishi wa Serikali, hii ni baada ya Serikali ya awamu
ya tano ikiongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuzitaka Halmashauri zote
nchini kukusanya mapato na kuacha kutumia wazabuni katika kukusanya mapato
kwenye masoko na minada.
MATUKIO KATIKA PICHA
Kutoka Kushoto Mhe. Juma Porini Keya, katikati ni Bw. Terry Hurson (Kaimu Mtunza Fedha) kushoto ni Charles Ghati (Mkusanyaji wa Mapato) katika mnada wa Rung'abure. |
Wafanyabiashara katika mnada wa kijiji cha Rung'abure wakifanya malipo. |
Huduma za chakula pia hupatikana. |
Mnatuhabarisha sawa ila mnadili saana na maswsla yabkiutendaji kumbuka nyie ni,wawakilishi wetu ingieni vijijini msiishie mjini na matukio tu chimbueni serengeti,muione kuna mapya kila siku yanatokea wengine tupo,mbali tunawategemea nyie mtuhabarishe
ReplyDeleteasanteni
nyakitono home