Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Mara zimehitimishwa Jumapili ya tarehe 21/08/2016 baada ya kuzunguka wilaya zote sita za mkoa wa mara na kukabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo. Mwenge wa Uhuru uliingia Wilayani Serengeti siku ya Jumamosi ya tarehe 20/08/2016 kupitia Kata ya Nyansurura, aidha mwenge huo ulizunguka wilayani na kuzindua miradi sita maendeleo yenye thamani ya jumla ya Tshs Milioni 755,437,611.00 na hatimae kukabidhiwa siku ya jumapili ya tarehe 21/8/2015 Mkoa wa Arusha.
Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge kwa Mwaka huu inasema kuwa VIJANA NI NGUVU KAZI YA TAIFA WASHIRIKISHWE NA KUWEZESHWA.
Viongozi mbali mbali kutoka Wilaya ya Serengeti tayari kuupokea Mwenge wa Uhuru
Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mhe. Nurdin Babu (Kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Tarime Mhe. Glorious Luoga.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa (kushoto) akiwasili katika kijiji cha Oloisakwaine kilichopo wilaya ya loliondo tayari kumkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa Ndg. George Jackson Mbijima Akiingia katika Wilaya ya Loliondo, Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mhe. Nurdin Babu (kushoto) Mwenge wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa tayari kuupeleka Mkoa wa Arusha. |
Mwenyekiki wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Juma Porini Keya
Msafara wa Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Serengeti kuelekea Wilaya ya Loliondo Mkoa wa Arusha.
No comments:
Post a Comment